Radio Waumini main Website:
Last update:

Habari

Habari

Habari

5 March 2008
HABARI ZENIT – KANISA 5TH MARCH 08 1.00PM Imefasiriwa na Nandika Amatieku Askofu mkuu Bruno Forte amehimiza kanisa kuangazia sehemu tatu za kuimarisha mawasiliano na mungu na matumizi ya lugha zinazowafikia watu leo. Askofu huyo wa jimbo katoliki la chieti-vasto, italy alisema hayo wiki iliyopita katika sherehe za kuadhimisha miaka arobaini za kitivo cha theologia huko catalonia. Alielezea umuhimu wa kuwepo kanisa katika muktadha wa utandawazi ili kukabiliana na ideologia huria. Wito wake kwa kanisa ulikuwa injili ihubiriwe katika nchi za magharibi, nchi maskini za kusini na kwa watu wote wa dini tofauti. Amezungumzia umuhimu wa umoja wa kikristu baina ya madhebu mbalimbali. Askofu huyo mkuu amesema tafakuri ya theologia kuhusu dini ni kielelezo cha utafiti wazi wa taaluma hiyo na wala sio tatanishi. Ameongeza kwamba dini nyinginezo zisizo za kikristu pia zina msingi thabiti wa ufunuo wa mungu na kwamba waumini wa dini hizo wanapata neema za mungu pia.
Powered by PhPeace 2.6.44